Sunday, August 30, 2015

MHE. FREDERICK SUMAYE ATOA YA MOYONI

Sumaye: Kwa ajili ya muda nitasema kwa kifupi sana, nimetoka chama cha mapinduzi, katibu mkuu alisema sisi ambao hatukuteuliwa hatukuwa na maadili, mimi nasema kama kipimo cha maadili ni mheshimiwa Kinana, mimi nitakuwa mtakatifu, CCM wamekuwa wakiongoza siasa ya chama kimoja kwa ngozi ya vyama vingi, mmekunjika kwa miaka yote.

Tulitaka kufanya mabadiliko kulekule, kukawa na tatizo ndani ya CCM, ukitaka kufanya lolote wanakuzingira.

Wanawajaza watanzania uoga wa usilolijua, mkiwapa wapinzani wataharibu nchi, kila binadamu ana uoga wa asilolijua. Lowassa kwa kuliona hilo, kwa kuwa watanzania wanamfahamu aliona uoga wa aina hiyo haitakuwepo, na mimi nimekuja kwa sababu hiyo. Watanzania leo elimu yetu inashuka sana, tunashusha alama za kufaulu wanafunzi ionekane wamefaulu wengi, pia ukienda katika afya. Tunataka tubadilishe hali hiyo.

Leo Lowassa ametoka CCM ameonekana hafai, lakini ni Kikwete aliyemfanya waziri mkuu wake, kuna Rais anaweka kiongozi ambae hafai? Lakini ni Lowassa huyuhuyu ndiye aliyemuingiza Kikwete Ikulu, Kwamba watanzania wanampenda Lowassa, halina mjadala.

Mmewasikia kwenye kampeni zao, fisadi mkubwa huyo amechukua fedha za matajiri, Lowassa amechukua ustaarabu wa kuwajibika. Waziri anachukua mzigo ili kumuokoa Rais na serikali yake. Asanteni sana.

Nyerere wakati anastaafu, kwenye kikao kimoja nafikiri cha halmashauri kuu. Alisema hajaona mtu mvumilivu kama Kawawa, alibeba mizigo aliyostahili kubeba yeye, ndiyo kazi aliyofanya Lowassa.

Vichwa vya treni vinavyonunuliwa, Lowassa alikuwepo? Wajenzi wa barabara nchi hii wanaidai serikali trilioni 1.4, kudai si tatizo katika hizo bilioni 900 ni pesa za adhabu, huo si ufisadi, mbona hawasemi? Serikali hii ni dhaifu sana na alituthibitishia katibu mkuu, mwenyewe kusema kuna mawaziri mizigo.

Mwisho wanalomsema nalo, Escrow Lowassa alikuwepo, kile kipande cha Rugemalira tulijua waliokula, kila kipande cha Habinder ni nani aliyekula, tangu lini benki ikaruhusiwa kutoa cash kwa mabilioni. Wamejenga kiburi, hawajali tena maumivu ya wananchi, naomba mwaka huu msikubali, watanzania mfurahie mabadiliko ya ndani ya vyama vingi.

Wanasema mgonjwa, mimi nataka niwaulize, kwani Magufuli mzima? Wanaenda kufanya nini Ulaya kama ni wazima, mtu yeyote ukishavuka miaka 50 hauwezi kuwa wazima kwa asilimia 100, hivi Rais Mkapa alipokuwa madarakani hakwenda kufanyiwa operashi Ulaya, nchi ilidorora? Alienda akarudi akaikuta nchi usalama.

Kwani Kikwete alivyokuwa madarakani hakwenda kufanyiwa upasuaji mkubwa Marekani, Rais si kazi ya kubeba zege Ikulu, anatakiwa kuwake timu nzuri ya kazi, yeye ni meneja tu, naomba sana tumchague itakapofika tarehe 25 Oktoba.

Asanteni sana, nawashukuru.

No comments:

Post a Comment