Monday, August 17, 2015

NAPE-Lowassa Amepewa Hiyo Nafasi ya Kugombea Urais Baada ya Kuinunua Kwa Viongozi wa Ukawa

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye amesema Lowassa hapendwi na wafuasi wa vyama vya upinzani, isipokuwa alipewa nafasi hiyo baada ya kuinunua kwa viongozi wa Ukawa, ambao wana tamaa ya fedha.
"Kila mtu anajua kuwa huyu bwana ameinunua hii nafasi kwa viongozi wa Ukawa, ndiyo maana watu wenye akili zao, wameamua kujiweka pembeni wamewaachia wenyewe na mzigo wao usiobebeka, inashangaza kuwa sisi tunawafukuza mafisadi wao wanawapokea, sasa wakipewa nchi si itakuwa hatari zaidi. Hivi umeshawasikia tangu ajiunge nao wanazungumza kuhusu ufisadi? Wanaona aibu kwa sababu katika nchi hii, ukitaja fisadi na mafisadi huwezi kumweka kando. Unafikiri Watanzania ni wajinga kiasi kwamba hawaoni huu usanii??” alihoji Nape

No comments:

Post a Comment