Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu (HESLB) imetangaza orodha ya waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo
2015/2016 ambao fomu za maombi zimegundulika kuwa na upungufu na
kuwataka kufanya marekebisho kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka
huu (2015).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Bodi hiyo leo (Ijumaa, Agosti 28, 2015), jumla ya fomu za waombaji wa
mikopo 7,788 kati ya 68,445 zilizopokelewa na kuhakikiwa zimegundulika
kuwa fomu zina upungufu na kuwataka waombaji kusoma majina yao katika
tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa
na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega, (Pichani) waombaji
ambao fomu zao zimegundulika kuwa na upungufu wanatakiwa kurekebisha
kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka huu (2015).
Kwa taarifa zaidi gonga kiungo hiki;
No comments:
Post a Comment