Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chadema,Rose Kamili,akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo jioni kuhusiana na tuhuma
alizozitoa mume wake kwamba waliishi kwa maisha ya kula mihogo na
familia yake ili kuhakikisha chadema inastawi na kuimarika jambo ambalo
si la kweli walikuwa na maisha mazuri ya kawaida tu na kusema kuwa
Dk.Slaa anapaswa awaombe radhi wataznzania kwa kufafanisha kula mihogo
kuwa ni umaskini na kuongeza kwa kusema mbona ukienda katika mahoteli
makubwa mihogo na viazi ipo na watu wenye pesa zao wanakula kama kawada.
akizungumzuia kuhusu matamshi aliyasema Dk.Slaa kwamba haongei na waziri
mkuu mstaafu,Sumaye,mama rose kamili alisema kuwa wiki tatu zilizopita
waziri mkuu huyo mstaafu aliomba namba za dk.slaa akampatia wakaongea
vizuri bila shida yoyote ila anamshangaa juzi aliposema mbele ya
waandishi wa habari kwamba hazungumzi na sumaye.
akizungumzia kuhusu kuja kwa lowassa chadema mama huyo alisema kuwa
Dk.slaa alikuwepo katika kumkaribisha waziri mkuu mstaafu,Edward Lowassa
kujiunga na chama hicho ni jambo la kushangaza akizungumza kwamba
hakushiriki na pia wakati chokochoko hizo za kustaafu ukatibu wake
alisema kuwa viongozi waandamizi wa chama cha mapinduzi walimfuata na
kumshawishi kutoludi kwenye ukatibu mkuu wake huo atapewa ubunge wa
kuteuliwa na rais atakayeapishwa na kupewa uwaziri katika serikali ya
awamu ya tano.
Kamili alimaliza kwa kutoa rai kwa watanzania wote nchini kutomsikiliza
Dk.Wilbrod Slaa na kuwasihi kuendelea kuwa na matumaini na mgombea wa
urais wa Chadema,Edward Lowassa aliyesimamishwa na chama chao pamoja na
umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) ili kukiondoa madarakani chama
tawala.
Linus Slaa.
Emiliana Slaa.
Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kushoto ni mtoto wake aliyezaa na Dk.Slaa aitwaye,Emiliana Slaa.
Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kulia ni mtoto wake, Linus Slaa.
waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini leo
Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Rose
Kamili, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu
ya mume wake Dk.Wilbrod Slaa kuzungumza wakati akiwa Katibu mkuu wa
chadema familia yake ilikula kwa shida kwa sababu ya kujenga chama hicho
jambo ambalo si la kweli. Wengineo ni watoto wake, Linus Slaa (kulia)
na Emiliana Slaa.
No comments:
Post a Comment