Watanzania
hususani vijana wametakiwa kukaa na kutafakari kwa kina mustakabali wa
taifa letu katika wakati huu wa uchaguzi na kuchagua viongozi ambao
hawatakuwa vibaraka wa mataifa mengine kutokana na Tanzania kuwa na
maliasili nyingi ikiwemo gesi na mafuta ambayo huenda mataifa hayo
yakautumia uchaguzi huu kuwaweka madarakani vibaraka wao na kuifanya
Tanzania kuwa muhanga wa maliasli zake kwa kushindwa kufikia malengo ya
kuwaondolea umasikini watanzania.
Hayo
yamesemwa na mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi CCM Dr John Pombe
Magufuli wakati akizungumza na viongozi wa ngazi za juu wa jumuia ya
wazazi Tanzania ambapo kupitia kwao amewataka kuwaelimisha vijana juu ya
kufanya mabadiliko ya pupa bila kujali athari za kesho kwa kuwa mjuto
ni mjukuu.
Aidha Dr
Magufuli ameendelea kusisitiza suala la kutunzwa kwa amani ya Tanzania
na kwamba watanzania wasikubali kufarakanishwa kutokana na itikadi ya
vyama vyao na kuwataka kumwamini kuwa ana uwezo wa kuleta mabadiliko ya
kimfumo ndani ya chama cha mapinduzi na serikali kwa ujumla kama china
ilivyofanya badala ya kufanya mabadiliko ya jazba kama nchi za Libya.
Mwenyeikiti
wa jumuia ya wazazi wa chama cha mapinduzi Alhaji Abdala Bulembo
amwakikishia mgombea huyo kuwa jumuia imejipanga kumsemea ili aendelee
kuaminiwa na watanzania kwani kazi alizozifanya zinaeleweka na
kuheshimiwa na watanania.
No comments:
Post a Comment