Saturday, August 22, 2015

CCM Yaanza na Mtaji wa Ubunge.....Mgombea Wake Mtwara Apita Bila Kupingwa


Jana ikiwa ndio  ni siku ya Mwisho kuchukua na Kurejesha Fomu za Urais,Ubunge na Udiwani Katika Majimbo Yote ya Uchaguzi Nchini,Chama Cha Mapinduzi Kimeanza Vema Harakati Hizo baada ya Aliekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Abdallah Dadi Chikota (pichani) kupita bila kupingwa kuwa Mbunge wa Jimbo jipya la Nanyamba,Mkoani Mtwara
 
Hatua hiyo Imetokea baada ya wagombea wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Na aliekuwa Mgombea wa Chama cha Wananchi CUF Kutojitokeza Kurudisha Fomu zao hadi Muda Uliopangwa na Tume ya Uchaguzi Kumalizika. Wagombea hao ambao walichukua Fomu na Kutorejesha ni Severin Simon Magwaya (CHADEMA) na Twahil Saidi Namwaga wa CUF.
 
Jimbo la Nanyamba katika Halmashauri ya Wilaya Ya Mtwara ni Jimbo Jipya Baada ya Kugawanywa Jimbo la Mtwara Vijijini Abdallah Dadi Chikota Ambae Hivi karibuni Aliagana na Wasaidizi wake wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Licha kuanza Harakati zake Za Kisiasa Aliwaomba Kutekeleza Vema Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Mkoa wa Lindi.
 
Chikota akibainisha Baadhi ya Miradi Hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Wodi ya Kisasa pamoja Nyumba ya Ghorofa itakayokaliwa na Familia  10 za Waganga katika Hospital Ya Sokoine Lindi,Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa
 
Kufuatia Kutotokea kwa Wagombea hao jana Sasa Inasubiriwa Taratibu za Tume ya Uchaguzi Kumtangaza Rasmi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mkoani Mtwara

No comments:

Post a Comment