MTANZANIA
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Vijijini kwa tiketi ya CHADEMA, Patrobas Katambi amevamiwa na kundi la watu wasiofahamika, wamemnyang’anywa Fomu yake ya Ubunge na kuichana.
Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justis Kamugisha
amethibitisha tukio hilo huku akisema tukio hilo lilitokea wakati
Mgombea huyo akiwa kwenye gari lake lililokuwa likiendeshwa na mdogo
wake.
Vijana hao walimvamia, wakamtukana
matusi na kumpora Fomu hizo pamoja na Fedha Ths, Milioni 2, Mgombea huyo
hakuumizwa wala kudhurika chochote wakati wa tukio hilo.
Mgombea huyo amesema Fomu zilizochanwa
zilikuwa ni kivuli (Photocopy), lakini Fomu halisi zilikuwa chini ya
siti ya gari ambapo vijana hao hawakuziona.
MWANANCHI
Jeshi la Polisi Tanzania limevipiga
marufuku Vikosi vya Ulinzi vya Vyama vya kisiasa kufanya kazi za ulinzi
hadharani kwa madai kuwa vinaingilia majukumu yao.
Onyo hilo lilitolewa jana na Kamishna wa
Polisi–Operesheni na Mfunzo, Paul Chagonja huku akivitaja baadhi ya
Vikundi hivyo kuwa ni Green Guard (CCM), Red Brigade (CHADEMA) na Blue Guard (CUF), ambavyo hutumiwa na vyama vya siasa katika mikutano yao.
Agizo la Chagonja
limekuja miezi minne baada ya agizo la Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP
Ernest Mangu kupiga marufuku vikundi hivyo vya vyama vya siasa ambavyo
vina muonekano na muundo wa vyombo vya usalama.
“Polisi
imejipanga vizuri kuhakikisha mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa
inafanyika katika hali ya utulivu hadi siku ya uchaguzi,“ alisema Kamishna Chagonja.
Akizungumza hatua hiyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema kuwa askari polisi hawatoshi kulinda mkutano wa watu wengi hivyo wataendelea kuwatumia kulinda wanachama wao.
Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema katika chama chao hakuna kikundi kinachoitwa Green Guard kwani hata Katiba ya chama hicho hakina watu kama hao.
Mkurugenzi wa uchaguzi wa Chama cha CUF, Shaweji Mketo
alisisitiza chama chake kuendelea kuwatumia kwa sababu wapo kikatiba na
katiba yao ilipitishwa na Serikali na inatambuliwa na msajili wa vyama
vya siasa.
MWANANCHI
Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Sekondari ya Nyasubi Shinyanga, Ally Jacob ameuawa baada kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni alipokuwa akijaribu kumwokoa mwanafunzi mwenzake asibakwe.
Tukio hilo lilitokea wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akirejea nyumbani kutokea shuleni… Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justus Kamugisha
alidai kuwa mwanafunzi huyo aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha
kali sehemu ya shingoni na mwenzake anayesoma Sekondari ya Kishimba.
Kamugisha alisema sababu za Jacob kuuawa
ni kujaribu kumsaidia mwanafunzi mwenzake mwenye umri wa miaka 16
ambaye anasoma kidato cha pili Sekondari ya Nyasubi ili asibakwe na
mtuhumiwa ambaye alitaka kufanya unyama huo kwa kushirikiana na mkazi
mmoja wa Nyasubi.
Alisema watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika
No comments:
Post a Comment