Staa wa Bongo, Nasibu Abdul 'Diamond'
KUELEKEA
Uchaguzi Mkuu wa urais nchini, wasanii Nasibu Abdul 'Diamond' na Ali
Saleh Kiba 'Aki Kiba' kesho Jumapili wanatarajiwa kutumbuiza katika
uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.
John Magufuli.
Diamond na Ali Kiba
ni sehemu ya wasanii wengi wa muziki na wale wa filamu watakaotoa
burudani kwenye uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika Viwanja vya Jangwani
jijini Dar es Salaam.
Staa wa Bongo, Ali Kiba
Kitendo
cha Ali Kiba na Diamond kupanda jukwaa moja ni nadra kutokea kutokana
na upinzani uliopo kati yao, hiyo watu watakaofika kwenye uzinduzi huo
watapata burudani ya bure ya aina yake.
Mbali
na kutamba na nyimbo nzuri kwa kila mmoja wao, kumekuwa na upinzani
mkali kuhusu msanii mkali wa kutawala jukwaa, hivyo wawili hao
wanatarajiwa kutoa burudani ya kiwango cha juu ili kuendelea
kuthibitisha ubora wao.
Magufuli
amepata nafasi hiyo baada ya kupita katika mchujo wa watangaza nia zaidi
ya 40 waliojitokeza ndani ya CCM. Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika
Oktoba 25, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment