Aliyekuwa Mwenyekiti
wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba akizungumza na
Wandishi wa habari katika moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Peacok
hotel jijini Dar leo kuhusiana na kung'atuka kwake rasmi Uenyekiti
wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida,ambapo Mh Lipumba
ameeleza kuwa yeye atabaki kuwa mwanachama hai na halali wa kawaida kwa
sababu kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020.
xxxxxxxxxxxxx
MWENYEKITI
wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa
Ibrahim Lipumba amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho leo majira ya saa
5 asubuhi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mbele ya waandishi habari,Pro.Lipumba amesema ametafakari sana katika
kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho lakini dhamira yake inamsuta.
Amesema kuwa
mwaka 2014 hakutaka kugombea nafasi hiyo kutokana na mchakato wa katiba mpya
akaamua kugombea kwa lengo ya kuwapa watanzania
katiba itakayoindoa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lipumba
amesema katika mchakato wa bunge maalumu wakaunda umoja wa katiba (UKAWA0 wenye lengo wa
kusimamia katiba iliyopendekezwa lakini sasa waliopitisha ndio wanataka
kuisimamia katiba hiyo ambayo haingii akilini.
Amesema
alikuwa akishiriki vikao vya UKAWA lakini Aprili 1 mwaka huu alisema atang'atuka
katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wanannchi (CUF).
Amesema
amepita katika misukosuko mingi katika kukijenga chama hadi kufikia kiasi hata kabambikiziwa
kesi ya kufanya maandamano bila kibali.
Lipumba
amesema kazi yake atakuwa mwanachama wa kawaida, kufanya utafiti wa maendeleo
endelevu pamoja na kufanya ushauri wa
masuala mbalimbali katika chama hicho. SOURCE:MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment