Na Yusef israel
Namshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuweza
kutufikisha hapa toka tupate uhuru na
toka nchi zetu mbili hizi zilizoweza kuungana na kuzaliwa taifa moja la jamhuri
ya muungano watu wa Tanzania,ni mambo
mengi tumeshuudia mazuri na mabaya
natunapakaa na kuangalia nyuma tunaona
kweli kuna mazuri tumefanikiwa na kuna mambo ambayo tumeshindwa kuyatimiza au
kuyatenda kwa sababu zetu wenyewe au makosa yetu wenyewe au sababu ya kutokuwa
na uwezo wa kifedha.
Tanzania ya leo in wananchi waliozaliwa
wakati nchi ikiwa inaitwa Tanganyika na
ikiwa haijapata uhuru na watanzania wa baada ya uhuru na Wa Tanzania wa walio zaliwa nchi ikiwa
inaitwa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ,je wakati nchi hizi zilizokuwa zinaungana Wazee wetu
walifikiria nini au nini kilichowafanya wazee wetu hawa waamue nchi izi mbili
ziungane utakuta kuna mambo mengi
yanayosemwa ,wengine ni kwa ajiri ya ulinzi wa visiwa hivyo visije
vikachukuliwa tena na sultan wa oman wengine hiyo ni siri ya Mwalimu na Mzee Karume kuna mambo mengi sana
na baadhi ya viongozi wa siasa waliosomeshwa na serikali zilizokuwa zikiongozwa
na wazee leo wamewaita majina mengi tu ya ajabu na kuwadharau.
Tukiangalia
kwa kirefu historia ya watu weusi wa Afrika mashariki utakuta tuna historia
ndefu sana na baadhi ya historia kwa vizazi vya leo hawajui,kutokana na historia
yetu ya kutawaliwa na kufanywa watumwa kwa zaidi ya miaka na miaka na waarabu
walikuja na kuleta dini kutoka uarabuni mpaka congo waliweza kutufanya kuwa
watumwa na kuwatumikia na kutuuza mpaka india ya kusini ndio maana ukienda
india ya kusini utapata waafrika ambao wanaitwa sidi hawa asili yao ni
msumbiji,Tanzania bara na visiwani na Mombasa
mpaka Somalia, ni hivyo hivyo katika dini ya wakristu Wazungu hawa walio
tuletea dini ya ukristu utakuta katika sehemu zingine za Africa mchezo ulikuwa ni huo huo kuanzia west Africa mpaka
Africa ya kusini ndio maana leo wafrica wameajaa latin America na visiwa vya
caribean ulaya ya magharibi na marekani.
Kwa kifupi kufatana na historia hiyo na
baada ya kuwapokea hawa watu na dini walizo tuletea na kuzipokea na kupewa
majina yasiyo yetu ya kiarabu na kizungu tumekuwa tukiishi kwa Amani na wakati
mwingine tumeweza kugombana au kutokea michafuko ya kidini katika nchi zingine
za ki Africa au vita za ukabila .kwa
kuangalia mbali wazee wetu waliamua kuangalia mbali sana kutokana historia ya
yetu sisi waafrica ndio maana wakaweka
uzalendo na kujithamini kwanza kwamba sisi ni waafrika kwanza na sisi ni watu
weusi kwanza ni lazima tuelewe hilo kwanza tuweke uzalendo na uafrica wetu
mbele kwa kizungu( Value)kwanza na ndio walipo angalia na kusema tuungane
tufanye taifa moja na ndipo kuzaliwa
Taifa laTanzania nia yao hawa wazee
ilikuwa ni nzuri sana na muungano ulifanyika katika kipindi kigumukwani dunia
ilikuwa iko na sehemu mbili ya Urusi na upande wa Amerika.
Wakati wasomi hawakuwa wengi lakini walisimama imara na kujenga taifa
lenye lugha moja Kiswahili,taifa lisilo na udini bali taifa la watanzania taifa
lisilo na ukabila taifa ambalo linaendeshwa na katiba yenye misingi binadamu
wote ni sawa na serikali aina dini bali
dini ni yako wewe mwenyewe unaweza kuwa muislam au mkrisitu,au kuwa mtu ambaye
auna dini.
Na ndiyo misingi mikubwa katika
demokrasia serikali aina dini na hiyo
imetokana na jibu ambalo Yesu aliwajibu cha mfalme ni cha mfalme nacha Mungu ni
cha Mungu na ndio ukawa ni mwanzo wa wa kuwa na serikali ambayo aina dini
pamoja na kuwa na wafalme au tawala ambazo hazikuweza kuanza kutenganisha utawala wa dini na serikali
lakini baadaye walikubali na kuanza
kutenganisha dini serikali pamoja na hayo bado kuna nchi zinatawaliwa na udini
uwezi kuwa au kupata cheo lazima wa dini hiyo kwa mfano uarabuni ,katika karne
hii ya leo hili jambo ndio mojawapo ya nguzo za demokrasia,
Ndugu zangu tumefika aje hapa tulipo imekuwa ni safari ndefu yenye milima na
mabonde imekuwa ni safari ya kupanda na
kushuka na baadaye na baadaye kuja kuonekana ni safari ya matumaini au
safari itakayo kuwa na manufaa mwaka
1967 Azimio la Arusha lilikuwa ni azimio la kuifanya Tanzania iwe nchi ya
kujitegemea sababu mwalimu alikuwa akiangalia mbali nchi aiwezi kuwa nchi ikiwa
inategema vitu kutoka nje au misaada au nchi iwe inaongozwa lakini aina uchumi
wa kujitegemea nasiyo kutegemea misaada na kuweka miiko ya uongozi na ndio maana lilikuwa
na mambo mengi mazuri na mambo mengine ambayo kama alikosea au walikosea leo
kuna wasomi wengi ambao wange weza kuyarekebisha sababu hakuna mtu mtakatifu
hapa duniani na hakuna kiongozi asiye kuwa na makosa au aliye weza kutekeleza
yote anayokusudia au aliyo aahidi lakini utakuta kwamba kila kiongozi
amechangia kitu Fulani katika maendeleo au kurekebisha kilicho kuwepo na kukifanya kuwa boro zaidi
na siyo kukivunja .
Mwaka
1979 mwalimu alisimamaimara katika vita ya kumtowa Iddi Amini
alipovamia
Tanzania na baada ya hapo ali ikawa si
nzuri kutokana na serikali kuweza kutumia pesa nyingi nawaliokuwepo
wakati huo watakumbuka tulikula unga wa njano sukari ya mstari sabuni
ya mstari lakini
pamoja na hayo yote Mwalimu alisimama imara katika kuongoza nchi na
chama mpaka
mwaka 1985 alipoachia madaraka lakini alipondoka aliacha nchi ikiwa na
viwanda
vingi shirika la ndege, shirika la reli ,shule
hospitali nchi ambayo aina udini wala ukabila nchi ambayo haina sisi ni
wakusini sisi ni wa kaskazini au sisi
ni wabara lakini leo haya mambo
yameoneka na udini umeingia katika siasa kama mlivyomsikia katibu
mstaafu wa
chadema alivosema juzi,
Je tunapokwenda tunapajuwa ?ningependa sana katika wakati huu wa
uchaguzi naomba niwakumbushe mkumbuke ya
kwamba kujenga ni ghali lakini kubomowa ni rahisi naomba sana viongozi wa siasa
wa ukawa na wa vyama siasa na ccm mkae
makini sana msitumihe lugha zitakazo leta umwagaji wa damu nakumbuka kwenye
bunge la Katiba Mheshimiwa lipumba aliwaita wana CCM itarahamwe ningependa sana
wana ukawa mkumbuke hilo neno baadhi yetu tulifiwa na ndugu zetu na rafiki zetu
kule Rwanda waliouliwa na hawa intarahamwe leo hii mnasema Mzee Mkapa kawaita
watu wa ukawa eti wapumbavu nawaomba
sana muepuke lugha za kipumbavu kabisa asala ya ni kubwa mambo yanapoharibika
wenye kupata shida huwa ni kina mama wazee na watoto hawa viongozi uwa wa
kwanza kupanda ndege nakukimbia naomba
mufanye siasa zenye ustaarabu na zenye ukweli na sio kupotesha umma sababu
baadhi ya wana siasa wamekuwa wana ukabila na wanaudini na waongo na wenye uchu
ya madaraka.
Ndugu watanzania najuwa mnataka mabadiriko na mimi pia nataka
mabadiriko lakini mabadiriko nayoyataka ni mabadiriko ya kiongozi amabaye ana makundi kundi lake ni
Tanzania kiongozi ambaye ni mchapa kazi,
kiongozi mwenye msimamo,kiongozi ambaye ana ukabira ,kiongozi ataye chaguwa
mawaziri wachapa kazi,mawaziri wenye uwezo wa kuongoza wizara zao kikamilifu
,kiongozi ambaye anauwezo wa kukemea kwa sauti ya ali ya juu kiongozi mwenye
kuamua maamuzi magumu,kiongozi ambaye atazifanya taasisi za serikali ziweze
kufanya kazi kwa ufanisi wa ali juu na bila kuingiliwa na kiongozi yoyote maana
yake akuna aliye juu ya sheria,kiongozi atayelinda na kuakikisha mali asili
inalindwa na inawanufaisha watanzania wote na kuirudia upya mikataba yote kwa
manufa ya watanzania sababu hapa Europe kila mwaka wakati wa summer waarabu
wankuja kupumzika kutoka hizo falme zote za kiarabu zenye mali asili ye mafuta
na gesi na unaona vile hawa jamaa wanavyonufaika na mali asili unaona vile
wanavyo sukuma watoto wa kuja kusoma
hapa ,kiongozi ataye tegeneneza mifumo
mizuri ya uwekezaji yaani miundo mbinu ,bara bara,umeme,maji,plan za miji na
sehemu za kuweka viwanda kiongozi
atayejenga highways kutoka Dar mpaka boda ya Uganda
,Zambia,Burundi,Msumbiji,,Congo,
Kwa muda wote nimekaa nikitafari je baada
ya pata shika ya bunge la katiba kuweza kuandika katiba yenye mawazo ya watu
wote wa vyama vya siasa je baada ya hao
jamaa kutoka ndani ya bunge tunaweza kupata katiba yenye manufaa kwa taifa je
raisi wa awamu ya tano hataweza kuwa mjasiri
na kusimama na kuangalia mbali au kuwa na vision kusema katiba hii
iliyopendekezwa inatakiwa iangaliwe upya au irekebeshwe ndipo hapo nilipoangalia kwa mbali na kuona
kinachotusumbua au kutuvuluga ni maendeleo na njaa ya uchumi na ndipo nikatapaza wazo hili hili muungano
huu uwe imara kwa kizazi na kizazi je tunaweza kuwa na katiba ya namna hii
Kiongozi mkweli mpinga rushwa kiongozi
atayeweza kukaa na kuangalia nchii inapashwa kuwa na katiba yenye maadili ya
ukweli katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania yenye serikari moja na Raisi mmoja na makamu wa Raisi pamoja
na mawaziri 8 na mawaziri wakuu wawili
waziri mkuu wa Zanzibar mwenye kuongoza wizara 14 na waziri mkuu wa serikali ya Tanzania bara mwenye
kuongoza mawaziri 14 yaani serikali yote ya jamhuri itakuwa na
mawaziri 36 ukiweka Raisi na makamu wake ni serikali yenye watu38 tuu.
Mawaziri hawa wakuu watakuwa na asilimia 50
ya nguvu ya kuamua mambo ya ndani au ya sehemu wanazoongoza katika maswala ya kiuchumi na kuakikisha
sehemu wanazo toka zinapata maendeleo na wanauwezo wa kwenda nje na kuomba
misaada na siyo mikopo nawala si mambo
ya ulinzi au mambo yanayousiana na uhusiano wa kimataifa watakuwa kutakuwa na
bunge bara na bunge la Zanzibar halafu bunge la jamuhuri la muungano ambalo
litakalo kuwa linakutana marambili kwa mwaka.
Kwa vile leo tuko na wasomi wengi waliosoma
najuwa palipo na nia pana njia kamatukipata raisi mchapa kazi mwenye uchungu na
nchi yake na siyo uchu wa madaraka raisi ambaye anajua mwafrika anasamani kama
watu wengine mwafrika astaili kuitwa tumbili sababu ya rangi yake mwafrika
apashwi kuuza mali yake bali wanaoitaka waje wajenge viwanda mwafrika anaitaji
hospitali,maji,barabara,shule,nyumba bora,mwafrika anaitaji ulinzi na amani
,mwafrika anaitaji uongozi wenye maadili uongozi ambao hauna ukabila,udini
wenye msimamo ,
Tutaweza kupata katiba ya haki naya ukweli
namini watawezakukaa na kutengeneza katiba yenye kuleta maendeleo visiwani na
bara itakayonufaisha watu wa jamuhuri ya
muungano wa Tanzania.
Ninamengi ya kusema lakini leo nataka
niishihe hapa sababu unapotembea nje ya
nchi yako ndio unajuwa faida ya nyumbani au taifa unalotoka sisi wengine
tumeitwa tumbili au nyani na hakuna kitu kinauma mtu kukuita sababu ya rangi
yako au kukubagua sababu ya rangi yako
na wakati vitu walivyonao hawa wenzetu at kwetu vinawezekana kama tuna
uongozi thabiti na imara,
Watanzania chagueheni kiongozi makini chagueni kiongozi mwenye sifa za uchapa
kazi chagueni kiongozi atayeleta
maendeleo mapya na kuweka kasi katika uwajibikaji chagueni kiongozi asiye na
udini wala ukabila na hao viongozi wa
dini watoke kwenye siasa si ya kwao kabisa wakae pembeni kabisa,
Naomba vijana msindanganywe na baadhi ya
wanasiasa kuwatumia mkumbuke Libya,Syria,Rwanda DRC ,Uganda kabla ya Museveni ,Burundi,Tunisia,Iraq
maendeleo yanakuja kwa amani na si vurugu ninayasema haya sababu nimeshudia
vita mbili uso kwa uso macho kwa macho 1984 up 1986 Uganda na 1992 1994Rwanda
Mwisho naomba Azam TV au Tbc au Itv
watayarishe mdaharo wa watu wanowania uraisi na umakamu iliwaweze kujieleza
mbele ya umma, nini watawafanyia waTanzania sababu tumeonaawamu zote nne
kumekuwa na maendeleo lakini je wao watapo ingia madarakani nini watawafanyia
waTanzania au umasikini wataufukuzavipi?sababu umasikini ndio adui mkubwa
Na mwisho tume ya uchaguzi tunaomba
uchaguzi uwe wa wazi na amani na atayeshindwa akubali kwa uwazi,na kwa heshima,
No comments:
Post a Comment