Wednesday, September 2, 2015

HIZI NDIO KAULI 40 ZA DK SLAA JANA KWENYE MKUTANO WAKE NA WANAHABARI

1.Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutujali uzima.
2. Nimeamua kujitokeza leo hii ili kumesha upotoshaji na kuuweka wazi ukweli.
3.Sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia ninachokiamini.
4.Sina ugomvi na kiongozi yeyote maana siasa sio uadai.
5. Siasa inapoongozwa kwa misingi ya upotoshaji, matokeo yake ni vurugu.
6. Naweka wazi kuwa mimi sikuwa likizo na hakuna aliyenipa likizo yoyote.
7.Kilichotokea ni kuwa niliamua kuachana na siasa tangu 28.7.2015 saa sita usiku baada ya kutoridhishwa na kilichokuwa kinaendelea ndani ya chama changu.
8.Ni kweli nilishiriki kumleta Lowassa CHADEMA Lakini nilikuwa na misimamo yangu ambayo ilitufanya tusielewane.
9. Baada ya Lowassa kukatwa pale Dodoma, Gwajima ambaye ni mshenga wa Lowassa alinipigia simu kutaka kujua nii cha kufanya.
10. Nilimpigia Mwenyekiti Mbowe kumjulisha na tukakubaliana kupanga muda wa kuwasikiliza.
11. Kabla ya kuanza kuwasikiliza, msimamo wangu ulikuwa ni kumtaka Lowassa kwanza atangaze kuhama chama, aweke wazi ni chama gani anaenda na ajisafishe juu ya tuhuma zake



12.Tangu akatwe jina, Lowassa hakutangaza kujitoa CCM na wala hakujisafisha na tuhuma zake, kitu kilichonifanye nitofautiane naye.
13. Niliwauliza wanachadema wenzangu kuwa Lowassa anakuja kama Mtaji au Mzigo?
14. Swala sio urais kama watu wanavyozusha, mimi nilikuwa nataka mgombea mwenye uwezo na sifa ambaye ataweza kuitoa CCM. Sikuwa na tamaa ya urais kama watu wanavyosema
15. Tangu Gwajima atupe taarifa za ujio wa Lowassa, Swali langu la Lowasssa kuwa Mtaji au mzigo halikuwahi kujibiwa.
16. Nilitaka kujua ni mtaji gani lowassa atakuja nao na ni viongozi gan atakuja nao.
17. Nilijibiwa kuwa anakuja na wabunge 50 wa CCM, wenyeviti 22 wa mikoa na wenyeviti 80 wa wilaya.
18.Baada ya ahadi hiyo, nilitaka sasa nipewe majina ya hawa watu lakini mpaka tarehe 25 july sikupewa hayo majina
19. Wenzangu waliniambia kuwa tarehe 27 niitishe kikao cha dharura ila niligoma kwa sababu nilikuwa sijapewa haya majina
20. Ndani ya kikao hicho, tulianza kwa mabishano makali kati yangu na Mbowe, Lissu na Gwajima, viongozi wenzangu ni shahidi na mungu anajua. Msimamo wangu ulikuwa ni uleule kujua mchango wa Lowassa
21. Kikao kile kikavunjika, baadae tukaingia kamati kuu lakini bado msimamo wangu ulikuwa ni uleule. Baadae nikaandika barua ya kujiuzulu.
22.Profesa Safari aliichana ile barua.
23.Cha kusikitisha ni kuwa Kesho yake picha zikaanza kusambaa mtandaoni zikimuonyesha la lowassa japo viongozi wangu walizikana zile picha. Kibaya ni kuwa viongozi waliuficha ukweli
24. Kesho yake niliandika tena barua rasmi ya kujiuzulu.
25. Baada ya pale zikaanza propaganda za uongo zikimuhusisha hadi mke wangu eti kanizuia.
26. Naomba watanzania wajue kuwa mke wangu hakuwahi kunizuia kwa lolote, lkn hata angefanya hivyo sio mbaya maana hata yeye ni mwanaharakati mwenye uchungu na nchi hii.
27. Mke wangu aliwahi hadi kuumia wakati akipigania ukombozi wa nchi hii.....Lakini sio mbaya, familia yangu imezoea propaganda.
28. Kikubwa katika harakati ni credibility ambayo lazima uilinde na mimi sitaki jina langu liharibiwe na ni haki yangu.
29. Maslah mapana ya taifa ndiyo yaliyotufikisha hapa na sio maslahi binafsi.
30.Lowassa na wapambe wake ni waongo maana hakuna hata kipengele kimoja walichokitekeleza.
31. Tulitaka hao wabunge 50 waje kwanza kabla ya mchato wa uteuzi ccm
32. Napinga kuchukua makapi ya CCM kuyaita MTAJI.
33.Mtu kama Sumaye ni FISADI na nilikuwa siongei naye
34. Sumaye aliwahi kusema CCM wakimchagua Lowassa atahama chama. Leo Lowassa kawaje msafi??
35. Tulitaka Mtaji toka kwa Lowassa na sio MAKAPI
36. Wenyeviti walioletwa na Lowassa ni MZIGO na namjua vizuri. Akithubutu kunijibu ntamwaga UOZO wake wote
37.Nani asiyejua Guninita pia ni mzigo??
38: Nawataka viongozi wangu wanijibu ni mtaji upi walioupata toka kwa Lowassa.
39. Mimi ni Padri Mstaafu, sipendi siasa za uongo.
39. Ukisema unataka kuiondoa CCM ni lazima ujikumbushe misingi ya CHADEMA ambayo ilikuwa ni uadilifu. Leo chadema hii ina Uadilifu gani??
40. Namshangaa sana Lowassa eti kusimama mbele ya watu akijinasibu kuwa ni msafi.....kwamba mwenye ushahidi aende Mahakamani. Ni dhambi kupotosha watu.
41. CCM hawana ujasiri, ni waoga na ndiyo maana wamewalea watu kama akina Lowassa. Source. Mpekuz

No comments:

Post a Comment