Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, Dk Wilbroad Slaa, ametangaza rasmi kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kuwapokea baadhi ya waliokuwa wanachama wa chama tawala caha Chama cha Mapinduzi CCM akiwemo mgombea kiti cha rais wa mungano wa upinzani Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, Edward Lowassa.
Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu Dk. Slaa alijitokeza kwa mara ya kwanza Jumatano mbele ya waandishi habari tangu kuanza kwa mchakato wa kumpata mgombea wa UKAWA kupitia chama chake cha CHADEMA na kukikosowa chama chake na mgombea wake.
Dk. Slaa anasema kwamba chama chake hakikutekeleza makubaliano waliyoafikiana ya kuwapokea baadhi ya makada wa CCM akiwemo Bw. Lowassa.
Kiongozi huyo wa zamani wa CHADEMA amesema kwamba anasimamia ukweli na kwamba dhamira yake imemfanya ashindwe kumuunga mkono mgombea ambaye amekuwa akimtuhumu kwenye majukwaa
Dk.Slaa amesisitiza kwamba hatahamia chama chochote cha siasa kwa sasa bali ataendelea kutoa mchango wake kwa umma wa watanzania nje ya vyama vya siasa kwa kutumia vipaji vyake alivyojaliwa na mwenyezi mungu na kwamba hajajiengua CHADEMA kwa ajili ya kukosa kugombea Urais.
Akijibu tuhuma za Dk. Slaa mwansheria wa CHADEMA Tundu Lissu anasema anashanga kwamba kiongozi huyo wa zamani anadai hakubaliani na uteuzi wa mgombea wao kwa ajili ya kiti cha rais wakati yeye ndiye aliyepanga na kumleta Lowassa katika chama hicho.
Vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu hivi sasa vipo kwenye kampeni katika maeneo mbalimbali nchini baada ya baadhi kufanya uzinduzi rasmi jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment