Wednesday, September 2, 2015

MBATIA AJIBU MAMBO ALIYOSEMA DR. SLAA JANA

Mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia ameongea mchana huu na waandishi wa habari na kujibu baadhi ya mambo aliyosema Dr. Slaa

Mbatia: Napenda kuwaomba Watanzania tusimame wote kupata Katiba mpya ambayo ndiyo ajenda ya mgombea wetu Lowassa. ‪#‎MbatiaAnaongea‬

Mbatia: Watanzania naomba waelewe UKAWA tunasimamia utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji ndani ya Tanzania.

Mbatia: Wanasiasa hasa wale wa CCM Mwakyembe na Sita, wanaotaka midahalo waje waongee na mimi wasimsumbue Mgombea wetu Lowassa sio saizi yao.

Mbatia: Hivi ni ashiria kwamba CCM wameshindwa hoja, mara kuleta mambo ya udini, mara wanaibua hili mara lile. wanataka kuchafua amani yetu kwa kuigiza masuala ya dini

Mbatia: Wagombea wetu urais walikaa na Dokta Slaa alisema mimi ni bora kuliko wote,leo hii anasema hajawahi kutia nia,kweli?

Mbatia: Tukisema tuibue masuala yote na kashifa za kuuzwa kwa nyumba, kuna mtu atabaki salama?

Mbatia: Eti Lowassa akija ndani ya Ukawa atakuja na Wenyeviti wa CCM..hakuwahi kusema..kayasemea wapi?

Mbatia: Wewe unasema ni muadilifu ulipewa Milioni 500 mwaka 2008 unakuja kusema leo baada ya miaka 7? Tuwe wakweli.

Mbatia: Eti suala la rushwa zaidi ya miaka 7 usiripoti halafu uje useme leo, kusema uongo ni kazi sana.

Mbatia: Napenda kuwaomba watanzania wote ambao ni zaidi ya milioni 46, wasiruhusu nchi yetu ikaharibiwa na watu 100.

Mbatia: Wakenya walisema hata kama ana makosa, walisema huyo huyo tunamtaka, wakampigia kura na leo ni Rais wao.

Mbatia: Watu wachache wanaotaka eti kwa lolote lile lazima waendelee kubaki madarakani, tunasema hapana.

Mbatia: Lazima tufute mfumo huu uondoke tuwe na Tanzania mpya.

Mbatia: Napenda kuwaomba wale Viongozi wa dini walionewa kwa yale ya jana, wasamehe na waachane nayo.

Mbatia: Lowassa hajawahi kutamka kuwa nikija ndani ya UKAWA nitakuja na wabunge 50, wenyeviti wa CCM na Makatibu nk.

Mbatia: Kama hana faida haya mafuriko tungepata wapi? Nyota ya Lowassa inang'aa hata wafanye nini hawamuwezi huyu jamaa

Mbatia: Hatuna haja ya kuanza kumjadili, hiyo ni kulipasua Taifa la Tanzania kwa maslahi binafsi

Mbatia: Kilichotusikitisha ni yeye kuhusisha watu wengine wasiohusika kwenye jamii yetu, viongozi wa dini wenye heshima zao, acha sisi vyama vya siasa tusuguane wenyewe.

Mbatia: Zimebaki siku 50 na kitu, haki itendeki na nchi yetu ibaki na amani siku zote

Mbatia: Anasema kaja kupambana na Lowassa kwakuwa anagombea urais, sasa Sumaye naye anagombea urais?

No comments:

Post a Comment