Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema wanaodhani wanatumika CCM wamekosa mwelekeo kwani alikuwa kinara wa kuitaka itoke madarakani.
Profesa
Lipumba aliyekuwa mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), alijiengua kwenye wadhifa huo kwa kile alichodai nafsi yake
itamhukumu kwa kumkaribisha kundini, Waziri Mkuu mstaafu, Edward
Lowassa.
Lowassa
aliyejiunga na Ukawa Julai 28, amepitishwa na vyama vya Chadema, NLD,
CUF na NCCR-Mageuzi kuwania kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 25.
Akizungumza
juzi usiku kwenye mahojiano maalumu na Kituo cha Televisheni cha Azam,
Profesa Lipumba alisema wanaosema wanatumika hawana hoja kwa kuwa
walipambana kuitoa CCM madarakani.
“Hivi
inaingia akilini kweli? Unapambana kuitoa CCM madarakani halafu hao hao
uliokuwa unawapiga, wakutumie kuitetea?,” alihoji Profesa Lipumba.
Akizungumzia
msimamo wake, Profesa Lipumba alisema dhamira yake inamsuta kuendelea
kubaki ndani ya umoja huo kwa kuwa bado anakumbuka mapambano waliyokuwa
wakiyafanya dhidi ya rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na uadilifu huku
akidai kwa sasa ajenda hiyo haipo tena kwenye upinzani.
“Hivi
wapinzani watazungumzia kuhusu ufisadi? wanasimamia wapi kwenye
uadilifu?,” alihoji Profesa Lipumba wakati akihojiwa kwenye televisheni
hiyo.
No comments:
Post a Comment