Mwanasheria
wa CHADEMA na mgombea ubunge jimbo la Singida mashariki, Tundu
Lissu,akizungumza kwenye mkutano wa kampeni ya Ukawa mkoa wa Singida
uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples mjini hapa.Pamoja na mambo
mengine,Tundu amewaomba wakazi wa Singida, kumpa kura ya ndiyo mgombea
urais kwa tiketi ya Ukawa, Edward Ngoyai Lowassa, wabunge na madiwani wa
Ukawa,ili kuigaragaza CCM kwa madai imechoka na umechuja mbele ya macho
ya Watanzania.
Mgombea
ubunge jimbo la Singida mjini kupitia ukawa, Mgana Izumbe Msindai,
akiomba kura kwenye mkutano wa kampeni wa Ukawa uliofanyika kwenye
uwanja wa Peoples mjini hapa. Msindai ambaye amewahi kuwa mbunge wa
jimbo la Iramba mashariki kwa vipindi vitatu mfululizo na mwenyekiti wa
wenyeviti wa CCM wa mikoa nchini,amewata wakazi wa jimbo la Singida
mjini kujitokeza kwa wingi oktoba 25 mwaka huu kuichana chana CCM kwa
kadi zao za kupigia kura.
MMwanafunzi
wa Chuo kikuu Dodoma na mgombea ubunge jimbo la Mkalama mkoani Singida,
mwenye umri wa miaka 22,Oscar Kapalale, akisalimia kwenye mkutano wa
kampeni Ukawa mkoa wa Singida,uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples mjini
hapa.Oscar ametoa tahadhari kwamba udongo wa sindano, lakini inao uwezo
mkubwa wa kuleta madhara kwa mtu mzima.
Aliyewahi
kuwa diwani wa CCM halmashauri ya manispaa ya Singida, Pantaleo
Sorongai,baada ya kushindwa kwenye kura za maoni,amekimbilia CHADEMA
kuchukua fomu ya kutetea nafasi hiyo safari hii kupitia tiketi ya
CHADEMA.Nyuma ni mwenyekiti CHADEMA mkoa wa Singida, Shaban Limu.
Baadhi ya wagombea udiwani katika manispaa ya Singida kupitia tiketi ya CHADEMA.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
SAKATA
la DK. Willibord Slaa la kujiuzulu nafasi ya katibu mkuu wa CHADEMA na
kuachana na siasa, limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa kitendo
hicho kimechangiwa kwa kiasi kikubwa na mke wake (DK. Slaa).
Akihutubia
mamia ya wakazi wa jimbo la Singida mjini, Mwanasheria wa CHADEMA
Taifa, Tundu Lissu, alisema imebainika kwamba Dk. Slaa hana nguvu yo
yote mbele ya mke wake ambaye inadaiwa hajafurahishwa na ujio wa
Lowassa CHADEMA.
Alisema
udhaifu wa Dk. Slaa umeonekana dhahiri baada ya kufukuzwa na mke wake
ndani ya nyumba aliyojengewa na CHADEMA na kusababisha alale ndani ya
gari usiku kucha.
“Maskini
Dk. Slaa, nyumba ambayo amejengewa na CHADEMA , kumbe ameisajili kwa
jina la mke wake. Baada ya kikao cha Kamati kuu ambacho Dk. Slaa
alikiitisha ambacho kilikubaliana kwa kauli moja ya ujio wa Lowassa.
Aliporejea nyumbani kwake na kumpa mke wake taarifa hii, mke wake huyo
alimwamuru aondoke mara moja ndani ya nyumba hiyo kwa madai sio ya
kwake”,alifafanua Tundu Lissu.
Alisema
kwa ujumla uamuzi huo wa kujiuzulu wadhifa wake wa ukatibu mkuu na
kuachana na siasa, haujatokana na dhamira yake bali unahisiwa umetokana
na mke wake kuchukizwa na kitendo cha Lowassa kujiunga na CHADEMA na
kupewa nafasi ya kugombea Urais.
Akifafanua, Tundu Lissu amesema Dk. Slaa ndiye mwanzilishi au mshenga mkuu wa harakati za Lowassa kujiunga na CHADEMA.
Alisema
mapema mei mwaka huu, Dk. Slaa alianza kumshawishi mwenyekiti wa
CHADEMA Freeman Mbowe wampokee Lowassa,kwa madai kwamba ni mtu pekee
mwenye nguvu ya kukisabaratisha Chama Cha Mapinduzi.
“Baada
ya Mwenyekiti Mbowe kukubaliana na ushawishi huo, kamati ya watu watatu
iliundwa na Dk. Slaa alikuwa mmoja wao pamoja na askofu Gwajima ambayo
ilipangiwa kukutana na timu ya Lowassa,kufanikisha lengo la
Lowassa,kujiunga na CHADEMA,kisha aweze kupeperusha bendera ya Ukawa
kusaka nafasi ya rais wa tano”,alisema.
Tundu
alisema kamati hiyo ya watu watatu katoka CHADEMA na ile ya Lowassa
ilifanya vikao karibu kila siku kwa kipindi cha miezi miwili mfululizo,
mwisho wa siku,kwa pamoja wanakamati hao walikubaliana na wazo la
kumpokea Lowassa.
“Baada
ya makubaliano hayo ambayo Dk. Slaa alikubaliana nayo toka mwanzo hadi
mwisho, aliitisha kikao cha dharau cha kamati kuu. Lakini kabla ya
kufanyika kwa kikao hicho, Dk. Slaa alibadilika ghafla na kuanza kudai
chama kimenunuliwa kizima kizima, na kwamba hakubaliani na kitendo
hicho”,alisema mwanasheria huyo wa CHADEMA.
Hata
hivyo,alisema nguvu kubwa ilitumika ikiwemo kumshirikisha baba yake
mzazi mwenye umri mkubwa, kumshawishi mwanae Dk. Slaa akubaliane na
maamuzi ya wengi, baada ya mazungumzo hayo yaliyochukua muda
mrefu,alikubaliana na maamuzi ya wengi.
Tundu
alisema Dk.Slaa aliporejea nyumbani kwake na kutoa taarifa kwa mke wake
kwamba wamekubaliana Lowassa agombee urais kwa tiketi ya Ukawa, ndipo
mwanamke huyo alipochukua uamuzi wa kumfukuza alipo ndani ya nyumba
iliyojengwa na CHADEMA na kupelekea katibu huyo mkuu wa zamani wa
CHADEMA,alale ndani ya gari lake.
Katika
hatua nyingine, Tundu Lissu ambaye amedai ameshirikishwa juu ya ujio wa
Lowassa kwenye hatua ya mwisho tu, alisema Lowassa alipoitwa na kamati
kuu ajisafishe juu ya ufisadi wa Richmond, aliiambia kamati kuu ya
CHADEMA, kuwa mhusika mkuu ni rais Kikwete.
“Katika
kujisafisha huko,Lowassa alituambia wakati tukio hilo linafanyika,yeye
alikuwa ni mtumishi mkuu wa serikali kazi yake ilikuwa ni kutekeleza
maagizo kutoka kwa rais na yale yaliyokuwa yanatolewa na vikao vya
baraza la mawaziri.Kimsingi tulikubaliana kwamba Lowassa kama
yeye,hahusiki na ufisadi huo”,alisema.
Baada
ya kufafanua kuhusu sakata la Dk.Slaa kwa takiribani saa
mbili,mwanasheria huyo alitumia fursa hiyo kumbombea kura Lowassa kwa
wakazi wa Mkoa wa Singida, ili kuiondosha madarakani CCM Kwa madai
kwamba imechoka na haina jipya tena.
No comments:
Post a Comment