Saturday, September 5, 2015

SentesI 10 Alizozisema Dr Slaa Usiku wa Jana kwenye Mahojiano Maalum Star TV


"Sina account Twitter, ila ninayo JamiiForums na Facebook ambazo ziko active".

"Watu walitumia picha yangu ya mkutano Mwanza na kusema Dr Slaa amerudi Ofisini".

"Watu wanatumia Picha zangu za zamani Mfano ile ya wakati Rais wa ujerumani amekuja, nilikuwa Na Mwigulu na Prof. Lipumba tukiwakilisha vyama vyetu".

"Picha nyingine nipo Kwenye ndege wakidai nakimbia nchi, Jambo ambalo sio kweli".

"Angalau huyu Magufuli anagusia ufisadi, lakini ushamsikia Lowassa na wenzie wakiongelea hilo?".

"Serikali ituambie hili deni la zaidi ya bilioni 90 tunamlipa nani? Maana kampuni haipo!"..

"WB na IMF na Wahisani sasa wanagoma kutupa pesa kwa sababu hatuaminiki".

"Kama mzazi mwenzangu anafanya shopping ili aongezewe dau, ila sio mimi Dr. Slaa".

Dr. Slaa amesema ili suala la sakata la Richmond lifikie mwisho inatakiwa Serikali ifungue kesi mahakamani na wale wote wenye ushahidi wakautoe mahakamani. Amesema yeye yuko tayari kwenda kutoa ushahidi huo kwa sababu anao.

No comments:

Post a Comment