HATIMAYE
chama cha ACT-waza lendo kimemtangaza Profesa kitala Mkumbo kuwa
mgombe wa Urais ndani ya Chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa hapo
baadae mwaka huu.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Vilevile pia chama hicho kimemtangaza Bi Haula Shamte kuwa mgombea mwenzi nafasi yaUrais.
Akitanga umamuzi huo leo Jijini Dar es Es Salaam,Katibu mkuu wa
ACT-Wazalendo Samson Mwigamba wakati alipokuwa anachukua fomu ya Urais
katika Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jijini dare s Salaama
ambapo amesema kwa sasa chama hicho kimempendekeza Profesa Mkumbo kuwa
mgombea wa Urais.
“Jumamosi Kamati kuu ya ACT-wazalendo kwa kauli moja tukafikia uamuzi wa
kumteua Profesa Kiitala Mkumbo pamoja na Bi Shamte kuwa wagombea wetu
wa juu ila ingawa kwa profesa kitila bado hajalizia uamuzi wetu ila
tunaimani atalidhia baada ya mazungumzo yetu ya kina”Amesema Mwigamba.
Mwigamba ameongeza kuwa sababu ya Kamati ya ACT-wazalendo kumteua
profesa Mkumbo inatokana na mchango wake ndani ya Chama hicho ,ikiwemo
kushiriki katika kutengeneza irani ya chama hicho pamoja na kuwepo
katika Kamati ya Uchaguzi na sera.
Mwanasiasa huyo machachari amebainisha kuwa chama hicho kimejipanga
kushinda katika uchaguzi huo mkuu unaotarajia kufanyika octoba 25 mwaka
huu kwa madai ya kuwa wagombea wote waliosimamishwa na vyama vingine
wanakashfa ya kubwa ya ufisadi huku akimtaja Mgombea wa Urais wa CCM
John Magufuli kuwa ni miongoni mwa wanasiasa wenye kashfa kubwa.
KUHUSU MADAI YA PROFESA LIPUMBA KUHAMIA ACT
Mwigamba
akusita kuzungumzia uvumi uliokuwa unaenezwa kwenye mitandao ya
Kijamii kuwa Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa
Ibrahimu Lipumba alitazamiwa kugombea nafasi ya Urais ndani ya
ACT-Wazalendo ambao Mwigamba amesema taarifa hizo ni za kutunga kwani
chama hicho,
Hakijampokea Profesa Lipumba lakini amedai chama hicho kitampokea kila mwanachama yoyote ambaye atafuata Sera na miongozo ya Chama cha ACT-Wazalendo.
Hakijampokea Profesa Lipumba lakini amedai chama hicho kitampokea kila mwanachama yoyote ambaye atafuata Sera na miongozo ya Chama cha ACT-Wazalendo.
VIJEMBE
Katibu
huyo wa ACT alikitumia lawama tume ya Uchuguzi nchini NEC kwa kitendo
chake cha kumfumbia macho Magufuli kwa kitendo chake anachodai cha
kufanya kampeni kabla ya mda kuanza .
.
UTATA WA KITILA MKUMBO
utata unazidi ibuka kwa mgombea huyo ambaye hapo awali alikuwa katika mipango ya kuhakikisha Edward lowassa anapita ndani ya CCM kwenye nafasi ya Urais,
utata unazidi ibuka kwa mgombea huyo ambaye hapo awali alikuwa katika mipango ya kuhakikisha Edward lowassa anapita ndani ya CCM kwenye nafasi ya Urais,
No comments:
Post a Comment